Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya wanawake ya Magereza imetwaa ubingwa wa mchezo huo  katika mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati  jana katika  uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar es Salaam.

Timu ya Magereza ya wanawake licha ya kufungwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Jeshi Stars wanawake kwa seti 3-2 walifanikiwa kuibuka mabingwa kwa tofauti ya pointi.

Kwa upande wa wanaume, timu ya mpira wa wavu (Volleyball) Jeshi Stars wamefanikiwa kuibuka mabingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kufanikiwa kuwafunga Magereza kwa ushindi wa seti 3-1.

Mabingwa hao wamekabidhiwa zawadi pamoja na kikombe na aliyekuwa mgeni rasmi Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja.

Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya Jeshi Stars, Fordey Edward ameibuka mchezaji bora (MVP)  wa mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati jana.

Fordey ameiwezesha timu yake ya Jeshi Stars kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya Magereza katika mchezo huo wa fainali. Fordey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Tabora pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya mchezo huo
 Nahodha wa timu hiyo Averine Albert akikabidhiwa kikombe na Mgeni rasmi Ndg. Ahmed Kiganja ambaye ni katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
 Nahodha wa timu hiyo ya Jeshi Stars Abel Masunga akikabidhiwa kombe lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...