Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto) akisaidia kushika kamba kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa soko Mlandizi.

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Mkoani Pwani, Hamoud Jumaa, amesema 2017/2018 anajikita kutekeleza ahadi na vipaumbele alivyojiwekea kwenye za huduma za kijamii hasa afya, elimu na soko. Katika utekelezaji huo, ameanza maandalizi ya kujenga soko la Mlandizi awamu ya kwanza litakalogharimu kiasi cha mil. 180 hadi kukamilika kwake. 

Jumaa alisema watafanya ujenzi kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itagharimu mil. 50. Alieleza kuwa, soko la Mlandizi ni soko linalotegemewa na wakazi wengi wa mji huo hivyo kuna kila sababu kulijengea mazingira bora na kuwa la kisasa. Aidha Jumaa alisema ,wafanyabiashara wamejipanga kumuunga mkono kwa kuchangia sh. 5, 000 kila mmoja ambazo zitakuwa zikichangishwa kupitia ofisi ya soko. 

"Simaanishi kuwa hakuna kero nyingine lakini ninafanya kwa awamu na mengine ninatekeleza pale napopata fedha ama wafadhili na wadau mbalimbali "alisema Jumaa. 

Jumaa alibainisha, masuala hayo ni utekekelezaji wa ilani ya CCM na atahakikisha hadi ifikapo 2020 awe amemaliza ahadi zake na vipaumbele alivyojiwekea.  Mbunge huyo alisema, ni jukumu lake kuwatumikia wananchi na aliwaomba washirikiane kwa kufuata kauli mbiu yake ya SISI KWANZAA SERIKALI BAADAE. 
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, akishiriki kuchimba mashimo ya maandalizi ya ujenzi wa soko Mlandizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...