Naibu
Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi muungano na Mazingira Mheshimiwa Luhaga
Mpina, amewataka wakazi wa Mkoa wa Morogoro kutunza Vyanzo vya maji na
Mazingira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameokoa maisha ya binadamu
na viumbe hai wengine.
Naibu Waziri Mpina ameyasema
hayo leo alipikuwa katika zoezi la usafi kitaifa Mjini Morogoro ambapo
amesisitiza kwa kufanya hivyo wakazi wa mkoa huo watakuwa wamesaidia
wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam Pamoja na pwani ambao vyanzo vyao vyingi
vya maji vimetokea mkoani Morogoro.
Mpina pia aliweka
msisitizo katika zoezi zima la upandaji miti ambapo kila wilaya
inatakiwa kupanda miti milioni moja na nusu, "kutakuwa na ufuatiliaji wa
hali ya katika utekelezaji wa zoezi hiyo katika ngazi ya Wilaya."
Alisisitiza Mpina.
Aidha Mpina aliunga Mkono Jitihada
za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika suala zima la utunzani na usafi wa
mazingira , "Mnae Mkuu wa Mkoa anaetosha, anaujua mkoa vizuri na hwa
ndiyo viongozi wa mkoa tunaowataka, wachapakazi na wenyekujituma.
Alisema Mpina."
Akiongelea suala la kuhamishwa
wananchi katika milima na vyanzo vya maji, NW Mpina Alisema kuwa "
Tunapowaondoa wananchi katika maeneo hayo aimaaninishi kwamba
tunawatesa. tunawapenda ndo maana tunawahamishia katika maeneo salama na
rafiki kwa mazingira, RC watoeni wananchi wanaokaa katika maweneo
Hatarishi." Alisema.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Bwana Kebwe Steven Kebwe, akizungumzia hali ya mazingira ya
mkoa huo, alisema kuwa mkoa utajitahidi kupambana na hali ya uharibifu
wa mazingira, pamoja na changamoto mkoa unazokumbana nazo akitolea mfano
upungu wa vifaa vya kuzolea taka.
Jumamosi
ya usafi wa Mazingira Mkoani Morogoro kwa Jumamosi ya Mwishho wa mwezi
wa nne ni utegelezaji wa Agizo la Mhe. Rais la Usafi wa Mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitoa Mchanga katika moja ya Mtaro Mijini Morogoro wakati wa kufanya usafi, Leo.
Kulia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwna Kebwe Steven Kebwe
akimkabirisha Naibu Waziri Mpina kabla a kuanza kwa zoezi la Usafi
kitaifa Mjini Morogoro siku ya Jumamosi ya Mwisho wa mwezi wa nne.
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitoa Mchanga katika moja ya Mtaro Mijini Morogoro wakati wa kufanya usafi, Leo.
Moja ya Mtaro Uliosafishwa katika zoezi la usafi wa mazingira leo Mjini Morogoro
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...