Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa msaada wa baiskeli na matibabu kwa Mwalimu Joyce Kantande ambaye alipata ulemavu kutokana na ajali aliyoipata akiwa na umri wa miaka saba.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa amesema wameguswa na tatizo la Joyce na hivyo uongozi wa hospitali umeamua kumpatia baiskeli hiyo ili kumwezesha kufanya shughuli zake akiwa amekaa .

‘’ Tuliona stori yake kwenye gazeti moja na kiukweli tumeguswa na tatizo lake kwani Joyce alikaa miaka 18 akiwa amelala baada ya kupata ajali iliyosababisha apate ulemavu kutokana na hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji Profesa Lawrence Museru ameona ni vema tukampatia msaada wa baiskeli, lakini pia kama Hospitali tutampatia msaada wa matibabu na tutakua tukimfuata na kumrudisha nyumbani kwa kipindi chote atakachokua akija hospitalini hapa kwa ajili ya matibabu,‘’ amesema Mtawa .

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Juma Mfinanga amesema kwa kushirikiana na wataalam wengine wa MNH watamfanyia vipimo mbalimbali ili kujua tiba gani anastahili .

Naye Mkuu wa Idara ya Tiba na Utengamao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Rosemary Kauzeni amesema watatumia utaalam wao kumsaidia Bi Joyce ili aweze kufanya shughuli zake akiwa amekaa badala ya kulala hususani shughuli zake za kufundisha watoto ambazo huzifanya akiwa amelala .

‘’Tutatumia utalaam wetu kwa kumpatia tiba ya mazoezi ya viungo ili aweze kukaa wakati anapofanya shughuli zake badala ya kulala na hatimaye aweze kutawala mazingira yake,” amesema.

Kwa upande wake Bi Joyce ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada alioupata na kuwaomba watu wengine kujitokeza kumsaidia kwani ana mahitaji mengi.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kumpatia Joyce Kanitande msaada wa baiskeli na matibabu ambayo yatamwezesha kufanya shughuli zake za kila siku. Joyce anatapatiwa matibabu katika hospitali hiyo baada ya kupta ajali na kuvunjika mgongo wakati akiwa na umri wa miaka saba.
Bi. Joyce akiwa amekaa kwenye baiskeli baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumpatia msaada huo leo.
Mkuu wa Idara ya Utengamano, Rosemary Kauzeni akiwaeleza waandishi wa habari jinsi Joyce akavyokuwa akipatiwa matibabu yakiwamo mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake.

Bi. Joyce akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako amefikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Joyce alipata ulemavu wa mgongo baada ya kupata ajali wakati akiwa na umri wa miaka 7 na hivyo kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...