Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameziagiza halmshauri zote za Mkoa wa Singida kuanzisha mabwawa ya ufugaji wa samaki ili kutunza mazingira, kuongeza kipato na kuwa darasa la kufundishia vikundi na wananchi wengine.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo mapema asubuhi ya leo katika shamba ya ufugaji wa samaki la Mikumbi lililopo manispaa ya Singida linalomilikiwa na Bwana Charles Kidua wakati wa uzinduzi wa mavuno ya kwanza ya samaki aina ya kambare katika mabwawa matatu kati ya sita yaliyopo katika shamba hilo.

Amesema halmashauri zionyeshe mfano kwa kuiga mbinu ya ufugaji wa samaki katika kutunza mazingira kwakuwa itaongeza kipato cha halmashauri pia halmashauri iangalie namna ya kufundisha ufugaji wa samaki vikundi vya vijana kuliko kuwapa mikopo ya pesa ambayo huishia kutumika vibaya.

Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa uwepo wa mabwawa hayo ya ufugaji wa samaki unaonyesha kuwa Mkoa wa Singida sio kame na wala sio mkoa masikini na uko tayari kuandaa chakula kulisha mikoa ya jirani hasa makao makuu ya nchi ambayo ni Dodoma.

“Tumejipanga na tuko vizuri kuhakikisha Dodoma inapata chakula kizuri na cha uhakika, Singida sio kame wala masikini, samaki hawafugwi kwenye ukame, Singida sio kame hata kidogo” amesisitiza Dkt. Nchimbi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kulia) akishiriki kuvua samaki aina ya kambare kwenye bwawa lililopo kwenye shamba la samaki la Mikumbi mjini hapa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi uvuvi kwenye shamba hilo.Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa mmiliki wa shamba la ufugaji samaki la Mikumbi Bw. Charles  Kidua (wa pili kulia) wakati akikagua shamba hilo lenye mabwawa sita yaliyofungwa samaki aina ya sato na kambare.
Mmiliki wa shamba la samaki Mikumbi mjini Singida na afisa maliasili Mkoa wa Singida Charles Kidua (aliyenyoosha mkono) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza kulia) muda mfupi kabla ya kuzinduliwa kwa uvuvi kwenye shamba hilo asubuhi ya leo.
Baadhi ya samaki aina ya kambare waliovuliwa mapema leo kwenye uzinduzi wa uvuvi shamba la samaki la Mikumbi lililopo mjini hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...