Serikali imewataka waajiri wote na wadau kwa ujumla kuhakikisha kuwa sehemu za kazi, mitambo na vifaa vya kufanyia kazi vinafanyiwa ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa havileti madhara kwa wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

“Kwa upande wa Serikali jukumu letu kubwa ni kuweka na kusimamia sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kutunga na kusimamia Sheria za Usalama na Afya Mahali pa Kazi, na kuweka viwango mbalimbali vya usalama na afya sehemu za kazi” alisisitiza Mavunde.

Mavunde alisema kuwa kwa sasa kanuni ya kuripoti ajali na magonjwa imekamilika na kuanza kutumika tangu mwezi Septemba, mwaka 2016.

Ambapo ameshauri wafanyakazi kuwasaidia waajiri wao kusimamia mifumo iliyopo, kujilinda wao binafsi ili wasiumie ama wasipate magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kutumia ipasavyo vifaa vyote vya kujikinga wawapo kazini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hotuba yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kuhusu  maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Aprili 25, 2017 Dodoma. 
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wakimsikiliza Naibu wake Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi hiyo ikiwa ni maandalizi ya ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Mjini Dodoma. 
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi. Khadija Mwenda akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa Mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...