Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa biashara zao.

BENKI ya NMB imekutanisha wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya wafanyabiashara wa NMB "NMB Business Club" kwa lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao. 

Kundi hilo la NMB Business Club mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa pamoja ili wafanyabiashara hao waweze kujuana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao jambo ambalo litachangia wao kushikamana na kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo. 

Akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo wataalam wa biashara wa Benki ya NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna ya kukuza biashara na kuelezea fursa anuai zilizopo ndani ya benki hiyo ili wateja wao waendelee kunufaika nazo. Alisema mbali ya kutoa mafunzo ya biashara na kodi wana NMB Business Club walioshiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya huduma wanazopewa ili benki iangalie namna ya kuzishughulikia. Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...