Wananchi
wa Mkoa wa Tabora wanakwenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya kunyeshewa mvua na
kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la Mahali pa
Kungonjea kuona wagonjwa.
Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.
Uzinduzi
huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi wakati wa
sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo Kitete.
Alisema
kuwa kukamilika kwa jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha
muda mrefu cha viongozi na wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu
kupumuzika wakati wakisubiri muda wa kuona wagonjwa wao wanapata
matibabu katika Hosptali hiyo.
Kaimu
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora
kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na
gharama nafuu.
Naye
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa ujenzi wa
jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo
Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia
miradi.
Alisema
kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo zilizosaidia
kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi hao na
hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando
ya barabara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...