Na Dotto Mwaibale, Chato

MAOFISA Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wameombwa kuwa weredi zaidi katika masuala ya kilimo ili elimu waliyonayo waweze kuitoa kwa wakulima ili nao waweze kulima kilimo chenye tija cha zao la mihogo ili zao hilo liweze kukubalika katika soko la kimataifa.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon wakati akitoa mafunzo kwa maofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi ya Teknolojia (Costech) kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

Alisema hivi sasa nchi ya China na Tanzania zimesaini mkataba wa ununuzi wa zao la muhogo jambo ambalo ni fursa kwa wakulima wetu wa hapa nchini wakiwemo wa kutoka wilaya ya Chato.

"Hii ni fursa kubwa kiuchumi lakini ni vema sasa tukaingia katika kilimo chenye tija ili mihogo yetu iweze kuingia katika soko la kimataifa badala ya kuendelea na kilimo kisicho na tija" alisema Simon.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akiwaonesha shamba la mfano la mahindi ambalo lipo nje ya ofisi yake wataalamu hao wa kilimo pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akionesha shamba la mfano la alizeti ambalo lipo nje ya ofisi yake. Kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Zao la alizeti likioneshwa.
Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF, Suleiman Okoth (wa nne kutoka kulia), akiwa na wataalamu hao wakilimo wakati wakiangalia bwawa la samaki la mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...