Wasichana 8,000 waliopo shuleni na 600 ambao hawako shuleni watanufaika na mradi mkubwa wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata elimu. Mradi huo wa miaka minne wenye gharama ya dola za Marekani milioni 5 utafanyika katika wilaya tano nchini. 

 Wilaya hizo ni Ngorongoro, Kasulu, Sengerema, Micheweni na Mkoani. Mradi huo ambao upo hatua ya pili umeanza kwa kongamano lililofunguliwa jana na Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo. Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akifungua rasmi kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Mradi huo mkubwa kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo umelenga kuwaokoa wanafunzi kabla hawajakumbwa na matatizo yanayokatisha masomo yao. Aidha utawapa fursa za kuboresha zaidi mafunzo mbalimbali waliyonayo ambao utawafanya kuwa watu wazuri zaidi katika jamii na hivyo kuchangia maendeleo ya taifa na jamii walizopo. 

 Katibu mkuu huyo ambaye alifungua kongamano na kuzindua mradi huoi awamu ya pili alisema kwamba ni matumaini yake kwamba jamii itaukumbatia mradi huo ili kuwa na taifa lenye mafanikio makubwa katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kwa kuzingatia lengo namba tano. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

 Amewataka wazazi na vijana kutimiza wajibu wao kwa kubadilika kitabia na kutambua umuhimu wa elimu katika kufanikisha wanachotaka ambacho ni maendeleo binafsi , familia na taifa kwa ujumla. Katika hotuba yake alisema ni matumaini kwamba wadau katika mradi huo watafaikisha katika kipindi cha miaka minne mipango yote iliyolenga kuboresha huduma kwa wasichana na wanawake vijana, kushawishi jamii kubadilika na kuachana na tamaduni mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji. 

 Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema mradi huo ulioanza mwaka jana na kufanyiwa tathmini umeonesha changamoto kubwa ya watoto wa kike ikiwamo mimba za utotoni,ukeketaji na kushindwa masomo. Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA) nchini, Joonsung Park akitoa neon kuhusu ufadhili wa KOICA ambao imeutoa katika mradi huo na mipango yao ya kusaidia Tanzania


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...