Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha za Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.

Taarifa ya Afisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imefafanua kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za serikali za Mitaa.

Mwakapiso, ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji wa sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)

"Huu ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG. Aidha kwa mujibu wa kanuni za ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu",alisema .

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe kutoka maktaba ya Kitengo cha habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...