Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.
Katika mazungumzo yao, Mhe Makonda na Bi. Cooke wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya majiji makubwa mawili Dar es salaam Tanzania na London nchini Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo Mhe MAKONDA ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.
Mhe MAKONDA pia ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya UTAMBUZ*I wa mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa zitakazofungwa *barabarani kwa ajili ya kusaidia USALAMA wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika jiji la London nchini Uingereza, hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji UWEZO kwa maofisa wa polisi wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.
Katika kukabiliana na changamoto ya MIGOGORO ya ARDHI mkoani Dar es salaam, Mhe MAKONDA ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo maafisa ARDHI na Mipango miji wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi, jambo litakalosaidia kuondoa KERO ya upatikanaji wa HATI pamoja na vibali vya UJENZI Mkoa wa Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimkaribisha mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar  na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...