KAMPUNI inayojishughulisha na uuzaji wa Vilainishi Duniani ( SINOPEC) imefanya Semina ya kuwaelimisha na kuwafundisha wateja wake mbalimbali namna ya kutumia ,kwa lengo la kulinda na kutunza Mazingira.

Akizungumza hayo mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Mkurugenzi mtendaji wa SINOPEC amesema kuwa,wameamua kuwekeza nchini Tanzania kutokana na Serikali ya awamu ya Tano,kupunguza vikwazo kwa wawekezaji kama ilivyokuwa awamu zilizopita.

" Kwa Afrika tumeanza kutoa Semina nchini Tanzania, yote hiyo imetokana na mazingira ya uwekezaji kuwa rafiki,hali nzuri ya Usalama pamoja na urafiki wetu wa muda mrefu na Tanzania" alisema Wang

Amesema kutokana kuweko kwa mazingira rafiki na wezeshi ya uwekazaji,wanaamini kampuni yake itajitanua zaidi kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania,ikiwa sambamba na kuhakikisha serikali inajipatia mapato stahiki kwa kulipa kodi .

Mkurugenzi huyo amewaomba Watanzania kwa ujumla wao kuvitumia vilainishi hivyo vyenye ubora wa Kimataifa,katika mitambo yao,mashine mbalimbali,magari na vifaa vinginevyo vinavyohitaji kutumia vilainishi.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SINOPEC, Jafali Mswahili amesema wateja wote pamoja na mainjinia watakuwa na utaratibu wa kupewa elimu ili kuwahikikishia wateja wao wanapata na kutumia vilainishi vilivyo bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SINOPEC, Andy Wang akionesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...