Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.


MAMIA ya wananchi wa mkoa Kigoma wamejitokeza katika kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika mpango unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF).

Matibabu hayo yanayotolewa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni yanahusisha magonjwa ya kina mama ,magonjwa ya moyo,magonjwa ya watoto ambayo madaktari bingwa wake watafanya kazi hiyo moja kwa moja huku magonjwa mengine ambayo hayana madaktari bingwa utatolewa ushauri wa hatua za kuchukua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo,Anne Makinda alisema kuwa hakuna mtanzania atakayekufa kwa sababu ya kukosa pesa za matibabu kutokana na serikali kuweka mfumo mzuri unaohakikisha wananchi wote wanapata matibabu kwa gharama nafuu.

Makinda alisema kuwa kwa sasa wananchi wote wataweza kujiunga na huduma za matibabu za mfuko huo kupitia makundi mbalimbali yalipo kwenye jamii na mitaa na wananchi watapata huduma za matibabu nchi nzima bila kubagua hospitali.

Alisema kuwa pamoja na hilo mfuko huo unatambua kuwepo kwa changamoto za uhaba wa madawa,vitendea kazi,uchache wa majengo na vifaa vingine vya kutolea tiba na kwamba mfuko huo umzingatia changamoto hiyo na kwa sasa mfuko unatoa mikopo kwa vituo vya afya,zahanati na hospitali ili kuwezesha huduma bora kupatikana wakati wote.
 Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya(NHIF) Anna Makinda akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika katika hospita ya Mkoa wa Kigoma (maweni) kwa ajili ya kupata huduma za madaktari bingwa. 
 Anna Makinda ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya (NHIF) akiongea na wagonjwa waliofika leo hospital ya Mkoa wa kigoma kwaajili ya kupata matibabu toka kwa madaktari bingwa.
 Anna Makinda akikata utepe katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma kuzindua zoezi la utoaji wa huduma kwa madaktari bingwa kwa hospitali za pembezoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...