Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imewaasa mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya kukutwa na meno ya tembo ya bilioni 5.4 inayomkabili Raia wa China maarufu kama 'malkia wa tembo' Feng Glan (66), na wenzake, kuheshimu mahakama, pindi inapopanga tarehe ya kusikiliza kesi hiyo

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi base's ya Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi kudai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba walikuwa na shahidi mmoja.

Nchimbi akadai washitakiwa wapo mahakamani lakini mawakili wanaowatetea hawapo licha ya kuwaona mahakamani hapo na kuzungumza nao kabla ya kesi hiyo kuitwa.

 Kutokana na hali hiyo, Hakimu Shaidi alisema amewasubiri mawakili hao ambao ni Jeremia Ntobesya na Nehemia Nkoko kwa  zaidi ya saa moja licha ya kuwa na majalada mengine ya kuandikia hukumu, ili waendelee na kesi hiyo lakini wameshindwa kutokea mahakamani.

Amesem ni mara nyingi upande huo wa utetezi umekuwa ukilalamika kwamba kesi hiyo haiendi kwa wakati  na kueleza kuwa leo shahidi ambaye alitoka Singida ameweza kufika.

 Hakimu shahidi akawauliza washitakiwa huenda hawajawalipa mawakili wao na wamefanya mgomo wa kuingia katika kesi hiyo kwa kuwa wameshindwa kutoa udhuru.

 Hata hivyo, Wakili Hassan Kiangio alidai kuwa shahidi aliyekuja ni kwa ajili ya mshitakiwa wa pili ambaye ni Philemone na kwamba anawakilishwa na Ntobesya na Nkoko ambao walikuwa kwenye kesi nyingine.

 Washitakiwa hao wamekanusha na kusema  wamewalipa mawakili wao na wanaomba muda kwa ajili ya kuwatafuta ili kuendelea na kesi kwani wanataka iishe.

Wakili Nchimbi, ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa ili washitakiwa waweze kuzungumza na mawakili wao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014  kwa makusudi  raia wa China, China, Yang Feng Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase  wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...