Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe
ametoa tahadhari kwa wawekezaji wote wa nje na ndani ambao hawana nia
njema na maendeleo ya taifa kuwa hawana nafasi nchini na kwamba
hawatapata fursa yoyote Tanzania.
Mwambe
ametoa tahadhari hiyo jana jioni katika kikao kifupi kilichoandaliwa na
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi kwa ajili ya kumuaga rasmi
Mkurugenzi huyo mara baada ya uteuzi wake ambapo hapo awali alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
Amesema
kituo cha uwekezaji kitashirikiana na wawekezaji wenye nia njema tu ila
wale ambao wanataka kujinuafiasha wao na kuliacha taifa bila faida
yoyote hawatapewa fursa yoyote ya kuwekeza nchini.
Mwambe
ameongeza kuwa atahakikisha kuwa wawekezaji wenye ubora na ambao
uwekezaji wao unamgusa mtanzania moja kwa moja wanapatikana hasa wale
ambao watasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kukuza uchumi.
“Nina
imani na wawekezaji wadogo ambao nitajitahidi kuwaunganisha na
wawekezaji wakubwa ili wakue na wajenge uchumi wa taifa itawasaidia pia
hao wawekezaji wadogo watapata uzoefu na hivyo kuwa wawekezaji wakubwa”,
amesema.
Mkurugenzi
wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia)
katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini Geoffrey Mwambe akiwashukuru
viongozi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano katika kikao kifupi cha
kumuaga.
Mkurugenzi
wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia)
katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...