Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Mbogwe watoe ushirikiano wa kutosha kwa Mradi Pendekezwa wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi (EACOP) linalotarajiwa kujengwa kutoka Ziwa Albert kupitia Kabaale (Uganda) hadi Rasi ya Chongoleani iliyo karibu na Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya ameyasema hayo alipofungua kikao cha maoni ya wadau (scoping) kwa Wakuu wa Idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kuhusu Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (TAM) ya mradi wa EACOP. Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Uganda (Ziwa Albert) hadi Tanzania (Tanga) lenye urefu wa kilometa 1445 linatarajiwa kupita katika wilaya ya Mbogwe. Akiongea wakati wa kikao hicho ,mwezeshaji kutoka kampuni ya JSB Envi-Dev Ltd Dr. Godfrey Kamukara ameelezea faida zitakazopatikana kutokana na mradi huo zikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa Mbogwe .

Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha mwingiliano wa makabila mbali mbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.

Dr.Kamukara amewataka watendaji kuwaelimisha wananchi kuhusu mafuta ghafi ili wananchi wasitoboe bomba wakidhani ni mafuta yanayofaa kwa matumizi . Alieleza kuwa mafuta ghafi ni mafuta ambayo bado hayajasafishwa kwa matumizi ya kawaida.

Kampuni ya RSK ya Uingereza na washirika wake kutoka Uganda ( ECO partners ) na Tanzania ( JSB Envi-Dev Ltd) wameanza kazi ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na mradi kwa kutoa maoni ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo. 

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...