Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa
ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220
linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Akizungumza
leo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara
ya Mayamaya-Mela KM 99.35, Naibu Waziri Ngonyani amesema kuwa kukamilika
kwa daraja hilo na barabara za maingilio katika daraja hilo
kutarahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani
ya Manyara na Arusha.
"Daraja
hili na barabara zake ni kiungo muhimu kati ya mkoa huu na mikoa ya
Manyara na Arusha na pia inaunganisha nchi ya Tanzania, (Cape Town)
South Afrika hadi (Cairo) Misri, hivyo kurahisisha huduma za usafirishaji
wa abiria na mizigo kutoka hapa kuelekea maeneo mengine", amesema
Eng.Ngonyani.
Aidha,
Naibu Waziri ameitaka kampuni ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza
daraja hilo ifikapo mwezi wa Kumi mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba
ili wananchi kuweza kulitumia.
Kwa
upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Eng. Leornado Licari, amesema kuwa
kwa sasa mradi umefika asilimia 87 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuweka
lami.
"Nakuhakikishia
kumaliza mradi huu kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache,
kwa hiyo hadi kufikia mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote",
amesisitiza Mhandisi Mshauri Licari.
Naibu
Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mikoa ya Dodoma
na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja hilo pia amekagua madaraja
mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela pamoja na ujenzi wa barabara
ya Mela-Bonga KM 88.8.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari.
Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimounesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 wakati alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga Km 88.8 Eng. Kini Kuyonza akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akikagua zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 eneo la Mlima Kolo uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...