Na,Vero Ignatus Arusha.
Katibu wa
CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda amekutana na
watumishi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo amesema
kuwa serikali ya awamu ya
tano inatambua na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya ,huku chama hicho kikiwa na
imani ya kwamba binadamu wote nisawa,heshima ,kutambuliwa pamoja na Ujamaa na
kujitegemea.
Ameyasema
haya leo katika kikao cha kuimarisha utendaji kazi na kuwataka
watumishi hao kuutanguliza
Uzalendo mbele,wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa na kwa Watanzania kwa
ujumla , kwa maadili na kwa usahihi.
"wakati
wa kupiga umekwisha,hatutakubali tumekupa uongozi hukuwa na mali
nyingi, ndani ya miaka miwili unakutwa unazo mali nyingi
ulizojilimbikizia bila kufahamika vyanzo vyake lazima tutakuhoji,kila
mtu atimize wajibu wake kwa kumuogopa Mungu" alisema katibu
huyo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro
amesema kuwa ni vyema kila mtumishi akasimamia eneo lake la kazi
ipasavyo bila kuingiza undugu kwenye kazi,kwani kila mmoja akisimamia
eneo lake kikamilifu hakuna mtu yeyote yule atakayekuwa na shida na
wao.
"Umepewa
eneo lako la uitumishi lisimamie ipasavyo usilete undugu kwenye
kazi,ukifanya kazi yako vizuri hakuna mwenye shida na wewe,unalipwa
mshahara ni vyema ukajiuliza je unafanya kazi kama ipasavyo?"alihoji
mkuu wa wilaya .
Aidha
Daqqaro amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi kwa moyo
safi,lugha nzuri ,kila mmoja afanye kazi yake kwa usahihi japokuwa
wananchi wengine wanakera ,amewataka kutambua kuwa mwisho wa siku wao
ndiyo wameajiriwa na siyo wale ambao wanawahudumia.
"Wahudumieni kwa moyo safi na lugha nzuri,tendeni kazi
kwa kuzingatia maadili na kwa usahihi,usije ukapigiwa simu na kiongozi
wako ukaanza kuingiwa na hofu na kujiuliza kuna jambo gani tena"
alisisitiza Daqqaro.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akiwa anazungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji katika Halmashari ya Jiji ,aliyepo kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro ,aliyepo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Kihamia
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na Watumishi wa Halamashauri ya Jiji la Arusha katika kikao hicho kilichofanyika leo
Baadhi ya watumishbi waliobhudhuria katika kikao hicho kilichofanyika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...