*Serikali kugawa salpha bure kwa wakulima wa korosho
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo Tanzania
(WMA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mizani katika maghala ya
kuhifadhia korosho ili kuepuka changamoto ya kutofautiana kwa uzito wa
bidhaa hiyo kila inapofikishwa kutoka katika vyama vya msingi.
Amesema
kitendo cha mizani za kwenye maghala hayo kupunguza uzito wa korosho
zinazopelekwa kutoka kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS)
hakivumiliki, hivyo Wakala wa Vipimo ipendekeze aina ya mizani
zitakazotumika katika upimaji wa korosho.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Mei 13, 2017) wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika katika
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
“Kuna
jambo baya sana linaendelea kila korosho inayofikishwa katika ghala kuu
lazima kilo ziwe zimepungua kwa zaidi ya kilo mia moja mpaka elfu, kwa
nini korosho tani kumi zikiletwa kwenye mizani yenu zinasoma tani nane
kwa nini?
“Na
huwa haitokei ikasoma tani kumi na mbili, wakati wote huwa inasoma
chini tu, watu wa WMA mpo fanyesni marekebisho, haiwezekani tukavumilia
wizi huu. Huna mkorosho hata mmoja lakini mwaka huu utasikia umeuza tani
zaidi ya elfu tano.Jambo hili lisijitokeze tena,” amesisitiza.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma .(PICHA NA OWM)
Wadau wa Tasnia ya Korosho wakimsikilza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho , Mama Anna Abdala baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini katikati ni Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Dr Chales Chizeba , Waziri Kuu amefungua Mkutano huo May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma.
(PICHA NA OWM).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...