Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni
katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day)
ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji
wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya
vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia
jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya
KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa
inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na
malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna
wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama
ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya
zoezi hilo.
“Tumeamua
kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani
katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.
Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki
ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga
mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la
damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza
kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo
peke yake.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu salama na kuipongeza Benki ya KCB kwa kushiriki katika zoezi hilo lililofanyika Makao Makuu ya benki hyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) kwenye picha ya pamoja na sehemu ya timu ya menejimenti ya Benki ya KCB Tanzania na baadhi ya wakilishi kutoka wizarani. Timu ya menejimenti ya Benki ya KCB, Wapili kulia ni Bw. Cosmass Kimario, wakwanza kulia ni Bw. Masika Mukule, wakwanza kushoto ni Bi. Christine Manyenye, wakwanza kushoto juu ni Bi. Joyce Wiki Mwashigadi na watatu kulia juu ni Bw. Rojas Mdoe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...