Shirika la Ndege la Kitanzania Precision Air limetangaza kuanzisha rasmi safari za ndege katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kupitia uwanja ndege wa Seronera. Safari hizo zitazinduliwa rasmi tarehe 1 Oktoba 2017. Tangazo hilo limetolewa huku shirika hilo pia likitarajia kuanzisha safari kati ya Tanzania na Uganda kupitia Uwanja wa kimataifa wa Entebbe mwanzoni mwa mwezi Julai.

Precision Air imekua ikafanya safari za kuelekea Seronera kupita utaratibu wa kukodishwa, na kuanza kwa safari hizi kutaifanya Precision Air kuwa shirika la kwanza ambalo ni mwanachama wa IATA kufanya safari za kwenda hifadhi ya Serengeti.

Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Robert Owusu amesema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maajabu saba ya Dunia na ni moja sehemu nzuri ambayo kila mtu hana budi kutembelea, na ili kufanikisha hilo Precision Air itafanya safari nne kwa wiki kati ya Dar es Salaam – Seronera na Zanzibar.

“Safari zetu kuelekea Seronera zinakwenda kufanya mapinduzi ya safari za kitalii. Sasa watalii watakuwa na uwezo wa kutua moja kwa moja ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kupata fursa ya kutumia mda mrefu zaidi ndani ya hifadhi, tofauti na awali ambapo walitumia muda mwingi barabarani. Ratiba ya safari zetu itakua kila siku ya Jumatatu,Jumatano,Jumamosi na Jumapili.” Ameeleza Bw.Owusu.

“Tunaamini kupitia safari hizi watalii wanaoitembelea Hifadhi ya Serengeti wataongezeka. Tumejidhatiti kutoa huduma za uhakika na kuchangia katika maendeleo ya utalii nchini.” Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama kampuni binafsi ya usafiri wa anga ikitumia Ndege aina ya Piper Aztec inayobeba abiria watano.

Mwanzoni Precision ilikua ikitoa hudma za usafiri wa anga kwa watalii waliokua wakitembelea vivutio vya mali asili katika hifadhi za Taifa za Serengeti,Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar na maeneo mengine nchini.

Shirika hilo limekua siku hadi suku na kuwa moja ya mashirika yanayoheshimika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika. Precision Air inafanya safari zake kutokea Dar es Salaam (makao makuu) kuelekea Arusha, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar and Nairobi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...