Na Bashir Yakub
Kwa kutumia kigezo cha usajili, Tanzania
tunazo aina kuu mbili za kampuni. Kampuni za ndani(Local companies) na
kampuni za kigeni ( foreign companies).
Kampuni za ndani ni zile zote zilizoanzishwa
hapa nchini na kusajiliwa hapa nchini. Hata kama wanahisa wake wote ni
raia wa kigeni kwasababu tu ya kuanzishwa hapa na kusajiliwa hapa zinakuwa ni
kampuni za ndani.
Kampuni ya kigeni ni ile iliyoanzishwa na
kusajiliwa nje ya Tanzania lakini ikaanzisha ofisi/biashara/tawi hapa Tanzania.
Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni kifungu cha 433 kinasema hivyo. Kampuni kama
imeanzishwa nje hata kama wanahisa wake wote ni Watanzania, hapa kwetu hiyo
bado ni kampuni ya kigeni.
Kampuni ya ndani inaposajiliwa hupatiwa
cheti cha usajili kiitwacho "Certificate of Incorporation" kwa mujibu
wa kifungu cha 15(2) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya ndani inapopata cheti hiki
basi usajili wake huwa umekamilika na inatambulika rasmi kama kampuni ya ndani.
Kampuni ya kigeni inaposajiliwa hapa
Tanzania hupatiwa cheti kiitwacho "Certificate of Compliance"
kwa mujibu wa kifungu cha 435(1) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya kigeni
inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na hutambulika rasmi
kama kampuni ya kigeni.
Acacia ni kampuni ya kigeni. Kwa maana
kuwa ilianzishwa nje ya Tanzania na kufungua shughuli zake hapa nchini. Kwa
hiyo ili ihesabike imesajiliwa Tanzania ilitakiwa kuwa na cheti
kiitwacho"Certificate of Compliance". Kutokuwa na cheti hiki maana yake
ni kuwa haijasajiliwa Tanzania na haitambuliki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...