Timu
ya wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wameanza maandalizi ya
uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Umeme Vijijini Awamu yaTatu (REA III)
katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Simiyu. Uzinduzi huo unatarajiwa
kufanywa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani mapema wiki
ijayo. Sambamba na uzinduzi huo, wakandarasi watakaotekeleza mradi huo watatambulishwa
kwa wabunge, madiwani na wanakijiji kutoka katika mikoa husika ambapo miradi
itatekelezwa.
Mkurugenzi
wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (wa
pili kushoto) akitoa maelekezo kwenye eneo la jiwe la msingi kwa ajili ya
uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambalo liko katika hatua za mwisho wa
ukamilishwaji wake.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera Mhe. Diwani Athuman (mbele) akizungumza na
timu ya watendaji kutoka Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na wakandarasi ofisini kwake kuhusiana na maandalizi
ya uzinduzi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu, Shaban Lissu (katikati) akisalimiana na
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), Elineema Mkumbo (kulia) mara baada ya timu ya maandalizi kuwasili katika eneo la
Rwabigaga wilayani Kyerwa ambapo kutafanyika uzinduzi huo kwa mkoa wa Kagera
Mkurugenzi
wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali
(kushoto) akielezea miradi ya umeme vijijini
inayotekelezwa na Wakala huo. Kulia ni Meneja Mipango Miradi na Tafiti kutoka wakala huo, Mhandisi Jones Olotu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...