Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Property
International, Abdul Haleem, kuhusu Ndege ya Kampuni hiyo inayopiga
picha za juu kwa muda mfupi wakati wa upimaji wa Viwanja (Unmanned Ariel
Vehcle As 1200) wakati Makamu wa Rais alipotembelea Banda la Maonyesho
la Kampui hiyo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,
akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Banda hilo. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, akiendelea
kutoa maelezo kwa Makamu wa Rais kuhusu ujenzi wa nyumba zinazojengwa
na Kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuuza na kukopesha Viwanja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Teknolojia ya 'Mega Panel' wa Kampuni ya Property International, Jonathana Kibona, wakati alipotembelea Banda la maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa la Kampuni hiyo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...