Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (wa pili kulia) akionyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis
Massawe (kulia), jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani humo ambalo limekwama
ujenzi wake mjini Babati mkoani humo. Mhe Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Juliette Sagamiko (kushoto) alipokua anatoa maelezo kuhusu Jengo la
Makao Makuu ya Uhamiaji mkoani humo (linaloonekana nyuma ya viongozi hao),
ambalo lipo katika hatua ya mwisho kukamilika lakini limekwama kuendelea na
ujenzi wake. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Afande Francis Massawe.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kushoto), akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara. Watatu kulia ni Kamanda wa Jeshi hilo,
mkoani humo, Heriel Kimaro. Masauni amemaliza ziara yake
ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya
Wizara yake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis Massawe, wakati alipokua akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Jeshi hilo ofisini kwake mkoani humo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...