Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George
Masaju ametoa wito kwa Asasi
zisizo za kiserikali ( NGO) kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili
kupitia ushirikiano huo kukomesha
na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania wenye albinism.
Mwanasheria Mkuu ametoa wito huo leo (
Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi Ikponwosa Ero, Mtaalamu Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albinism
“
Ningependa kutoa shukrani zako
kwa kuamua kuja Tanzania na kukutana na
viongozi mbalimbali wa Serikali, hii ni
fursa muhimu kwako ya kupata taarifa sahihi na rasmi
kuhusu jitihada , juhudi na mikakati
mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu
wenye albinism” akasema Mhe. Mwanasheria
Mkuu
Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe
basi uwahimize viongozi wa asasi zisizo za kiserikali
hususani zile zinazojihusisha na
watanzania wenye albinism
kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na
Ofisi yangu na Taasisi nyingine
za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la kuwasaidia
watanzania wenzetu”..
Akasema Serikali
inachukulia kwa uzito wa hali ya juu
makosa ya kijinai dhidi ya watu
wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia
wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na
sheria kuchukua mkondo wake.
Akasisitiza kwamba Katiba ya
Jamhuri ya Muungano imesisitiza
sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila
ya kubagua wakiwamo watu wenye
albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na
kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki
hiyo haimbagui mtu mwenye albinisim
au mtanzania yoyote ile na ndio
maana makosa ya jinai dhidi ya
haki ya mtu kuishi awaye yeyote
yule yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akifafanua kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Divisheni ya Mashtaka inavyoshughulikia kwa kupeleleza na kuendesha kesi za jinai dhidi ya watu wenye albnism. katika maelezo yake Mwanasheria Mkuu amesema Serikali inachukulia kwa uzito wa hali ya kipekee matatizo yanayowakabili watanzania wenye ualbino na kwamba juhudi hizo zimesaidia sana katika kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya jinadi dhidi ya watanzania hao ingawa bado kunachangamoto.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akimsikiliza Bi. Ikponwosa Ero, Mataalam Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albnism. Mhe. Mwanasheria Mkuu na Bi. Ero walikutana leo Jijini Dar es Salaam, ambapo walibadishana mawazo kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inavyoshughulikia matukio ya kijinai dhidi ya watanzania wenye albnism.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...