JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
Idara
ya Uhamiaji inapenda kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi
mbalimbali na Wageni wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa
Uhakiki ambao unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tz kabla
ya zoezi la uhakiki kuisha tarehe 19/07/2017.
Kwa
wale ambao kumbukumbu za vibali vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au
kuwa na tatizo lolote wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au
kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliotolewa.
Baada
ya kuisha kwa muda uliotolewa, Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na
kuwachukulia hatua za kisheria Wageni binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa
Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni wao watabainika kuwa na vibali
vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu wa utoaji vibali.
Idara
ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku 90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki
vibali vyao; tangu tarehe ya kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.
Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
14 JULAI, 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...