Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.
Hii inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo.
Alisema katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.Mpango wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.
Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.Kampuni ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...