Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati)
akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem (katikati) wakikabidhi kwa watoto
wenye matatizo ya moyo zawadi ya madaftari wakati wa hafla ya makabidhiano ya
vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini
Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza
na baadhi ya wazazi wenye watoto wenye matatizo ya moyo wakati wa hafla ya
kupokea vifaa tiba toka Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania Jasen Al Najem. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...