Na Rhoda James

Wizara ya Nishati na Madini imekutana na Kampuni ya Hyundai E & C ya Korea Kusini ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika vyanzo vipya vya nishati nchini.

Kampuni hiyo na Wizara wamekutana jijini Dar es Salaam ambapo kikao hicho pia kimehudhuriwa na taasisi zilizo chini ya Wizara likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Akizungumzia kuhusu uwekezaji huo, Kamishna wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile amesema kuwa Serikali inakaribisha wawekezaji zaidi kuwekeza nchini hususan katika vyanzo vipya vya umeme ikiwemo Makaa ya Mawe, miradi inayotumia nguvu za maji, pamoja na miradi ambayo bado haijaanza kutekelezwa.

Andilile ameeleza kuhusu miradi mikubwa ya nishati inayoendelea kutekelezwa nchini kwa sasa ikiwemo ile ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na kuitaja kuwa ni pamoja na Mradi wa Kinyerezi II wa Megawati 240, Kinyerezi I Extension Megawati 185.

“Ipo miradi ambayo inahitaji ufadhili au Serikali inahitaji kuingia ubia na Kampuni za ndani na nje ili kuifanikisha, mojawapo wa miradi hiyo ni Kiwira ambao Serikali ingependa kuona unaanza haraka,” amesisitiza Andilile.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Hyundai E & C, Dongil Chang amesema kuwa, kampuni hiyo inayo nia ya kuwekeza Tanzania kwa kuwa inao uzoefu mkubwa katika masuala ya Nishati.Ameongeza kuwa, kampuni hiyo ni ya 13 kwa ukubwa Duniani hivyo inavyo vigezo na uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali.

“Tupo tayari kuwekeza Tanzania katika sekta ya Nishati. Mara baada ya kupata taarifa zote muhimu kwa ajili ya uwekezaji bila shaka tutaanza majadiliano mara moja.” ameongeza Chang.
 Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile (wa kwanza kulia mstari wa mbele) ambaye ameeleza kuhusu uwekezaji katika masuala ya umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 18 Agosti, 2017 katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni wajumbe kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioshiriki kikao baina ya Wizara na Wawekezaji wa Kampuni ya Hyundai E & C.

Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifatilia mada katika kikao baina ya Wizara na Kampuni ya Hyundai E & C.

Kamishna wa Biashara nchini kutoka Ubalozi wa Korea, Jeon, Heesu (anayetoa maelezo) akielezea uzoefu wa Kampuni ya E & C katika masuala ya Nishati katika kikao kilichofanyika Wizara ya Nishati. Wengine katika picha ni Ujumbe kutoka Kampuni ya Hyundai E & C pamoja na Wawakilisha kutoka Benki ya Exim nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...