Na. Jeshi la Polisi.

Makamishna wastaafu wa Polisi Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke wametakiwa kuendeleza elimu ya Polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika maisha ya uraia baada ya kustaafu utumishi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa wahalifu hawapati nafasi ya kutamba hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga wastaafu hao lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.

IGP Sirro alisema kazi waliyofanya wastaafu hao ni kubwa lakini kustaafu kwao siyo mwisho wa kutumika katika kazi za Polisi na hivyo waendelee kuwa tayari wakati wowote kwa kuwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikisha jamii kukabiliana na uhalifu.

“Upolisi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na kwetu sisi tunaondelea kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote mazuri mliyofanya na nyie mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia kwa mawazo na milango yetu ipo wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama” Alisema IGP Sirro

Akizungumza baada ya kuagwa rasmi Jeshini Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Kamishna Mstaafu Paul Chagonja wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga makamishna wastaafu watatu, gwaride lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu. Kulia ni Kamishna Mstaafu Hamdani Makame.
Kamishna Mstaafu Paul Chagonja akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwaajili ya sherehe ya kuwaaga makamishna wastaafu watatu akiwemo kamishna Chagonja, Kmaishna Paul Chagonja na Kamishna Kenneth Kaseke. Gwaride hilo lilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.
Makamishna wastaafu Paul Chagonja (kushoto) na Hamdani makame wakisukumwa kwenye gari na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi katika kuwaaga maofisa wakuu. Makamishna hao wamestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria na waliandaliwa Gwaride maalum la kuwaaga lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam.Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...