Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu jijini Dar es Salaam.
 
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema kuwa, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji, anakesi ya kujibu dhidi ya tuhuma zake za kutumia dawa za kulevya.
 
Aidha Manji amedai anatarajia kuita mashahidi 15 watakaofika mahakamani hapo kumtetea.
 
Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya juzi, upande Wa mashtaka kufunga kesi kwa kuketa mashahidi watatu ambao no askari polisi watatu na mfanyakazi kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu.
 
Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkeha amesema, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka mahakama imeridhika kuwa mshtakiwa anahaki ya kujitetea.
 
Baaada ya kusema hayo, wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo alidai kuwa mteja wake (Manji) atajitetea kwa njia ya kiapo na pia ataita mashihidi 15 kwa ajili ya utetezi wake.
 
Pia Ndusyepo ameiomba mahakama kuwapatia hati ya wito kwa ajili ya Kuwaita mashahidi wao mahakani.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 30 na 31 kwa ajili ya mshtakiwa Manji kuanza kujitetea.
 
Katika kesi hiyo Manji anadaiwa kukutwa akitumia dawa za kulevya aina ya Heroine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...