Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA)ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zinazoshiriki maonyesho ya Kitaifa ya
Nanenane, yanayofanyika katika Mkoa wa Lindi katika viwanja vya Ngongo.
Maonyesho hayo ambayo
yamezinduliwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene;
ambaye amewasili na kukagua baadhi ya mabanda kabla kuwahutubia wananchi wa
Lindi waliokusanyika kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
NIDA inashiriki kwenye maonyesho
hayo kwa kutoa huduma ya Usajili kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi ambapo kwa wale
watakaokamilisha taratibu zote za Usajili watapatiwa Vitambulisho vyao ndani ya
mwezi mmoja. Huduma nyingine zinazotolewa ni pamoja na Ugawaji wa Vitambulisho
vya Taifa kwa wananchi ambao walisajiliwa kwenye maonyesho hayo mwaka Jana,
wananchi kupata taarifa za vitambulisho vyao kwa wale ambao wamekamilisha
taratibu za Usajili, elimu kuhusu matumizi, faida na umuhimu wa Vitambulisho
vya Taifa pamoja na kusoma taarifa za mwananchi kwenye Kitambulisho chake
kutumia Tovuti Salama iliyoundwa kurahisisha matumizi ya vitambulisho vya Taifa.
Kauli Mbiu ya maonyesho hayo kwa
mwaka huu “Zalisha kwa Tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili
kufikia uchumi wa kati”. Ili kufikia malengo haya; kupitia mfumo wa Taifa wa
Usajili na Utambuzi wa Watu kuwatambua Wakulima na Wafugaji, uzalishaji wenye
tija na ufugaji wa kisasa unawezekana. Hivyo wananchi wanahimizwa kujitokeza
kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa mapana ya mfumo huu katika kuinua
uchumi na maendeleo ya Taifa.
Maonyesho ya Nanenane Kitaifa
yanafanyika kwa awamu ya Nne mkoani Lindi ili kutoa fursa pana kwa wakulima na
wafugaji kunufaika na elimu pana inayotolewa na Taasisi na Mashirika mbalimbali
kwa lengo la kufanikisha ndoto kubwa ya Taifa la Uchumi wa Kati.
Mmoja wa wananchi wa Lindi akipata maelekezo toka kwa Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA, Bi. Rose Mdami.
Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika viwanja ya
Ngongo, karibu kabisa na Jukwaa Kuu la Maonyesho.
Baadhi ya Wananchi waliotembelea Banda la NIDA wakifuatilia
maelelezo ya namna ya kujisajili toka kwa Afisa Usajili mkoa wa Lindi Ndugu
Oliver Walles Mahinya.
Kikundi cha ngoma za jadi kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa
Maonyesho ya Nanenane Viwanja vya Ngongo Lindi.
Wananchi wa Mkoa wa Lindi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi
rasmi wa maonyesho ya Kitaifa ya Nananenane yanayofanyika mkoani humo kwenye
viwanja vya Ngongo. Maonyesho ya Nanenane yaliasisiwa mwaka 1990 mkoani Mbeya
na yameendelea kwa mzunguko kwa kila mkoa kupata fursa ya kuandaa na kushiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...