Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akizungumza wakati akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino wakati wa kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Itiso Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Na.Angela Msimbira

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa Mhe Seleman Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kumrudisha Mkandarasi na Mtaalam mshauri waliojenga mradi wa maji kijiji cha Itiso kilichopo Wilayani Chamwino kutokana na kujenga mradi huo kinyume na mkataba uliotolewa na Serikali na chini ya kiwango.

Mhe. Jafo Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa Itiso uliokuwa ukisimamiwa na Kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company Limited uliogharimu kiasi cha shilingi 338,676,323. Mhe. Jafo amesema kuwa Mkandarasi pamoja na mshauri wameondoka kwenye mradi kabla mradi kukamilika kitendo ambacho kinaisababishia hasara serikali ambapo fedha ambazo zilitakiwa kutumika kukidhi mahitaji ya wananchi zinapotea.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akikagua moja ya kichoteo cha maji wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Maji katika kijiji cha Itiso katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Mhe Jafo amesema hajaridhika na kazi iliyofanywa na Mkandarasi Audancia aliyejenga mradi wa maji kijijini Itiso kutokanana kulaza mabomba yaliyo chini ya kiwango na ni kinyume na mkataba aliopewa na Serikali.

“Nimesikitishwa na Mkandarasi wa Mradi wa Maji Itiso kwa kuwa amelaza mabomba yaliyo chini ya kiwango tofauti na mkataba aliopewa na Serikali na kusababisha wananchi wa kijiji cha Itiso kukosa kupata maji kwa wakati na kurudisha nyuma juhudi za serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amesema Serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili iweze kutekeleza miradi ambayo itasaidia wananchi lakini miradi mingi hujengwa chini ya kiwango na kutokamilika kwa wakati na hivyo kurudisha nyuma maendeleo kwa wananchi.

“Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kujenga miradi ya maji lakini miradi mingi imekuwa haikamiliki kwa wakati na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa serikali haitimizi ahadi zake“ Amesema.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo akimsikiliza Fundi Sanifu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Stephen Mzuri akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kisima cha Maji kilichopo katika Kijiji cha Itiso Halmashauri iya Wilaya ya Chamwingo.

Amewaagiza watumishi waliopewa dhamana yakusimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatumia weledi wa kazi yao kuhakikisha  miradi yote  ya  Serikali inamalizika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa na waache kufanya kazi kwa mazoea. “Watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia Miradi ya Maendeleo wanatakiwa kutimiza wajibu wao katika kuleta maendeleo kwa wananchi”

Akisoma taarifa ya Mradi wa Maji Itiso Fundi  Sanifu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Stephen Mzuri amesema Mradi wa maji Kijiji cha Itiso ulianza kujengwa mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2014 na kujengwa na Kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company L.T.D uliogharimu shilingi  milioni 338,676,323/=.

Amesema kuwa kulingana na mkataba Mkandarasi alitakiwa kulaza mabomba ya Class C kwenye laini inayotoa maji kwenye kisima na kupeleka kwenye tanki lakini mkandarasi alilaza mabomba ya class B. Pia kuvuja kwa maji na vichoteo viwili kati ya vichoteo nane havikuwa vinatoa maji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akikagua mashine ya kusukuma Maji kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji katika kijiji cha Itiso katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Bw.Mzuri amesema mpaka sasa vichoteo vitano kati ya kumi vinatoa huduma ya maji kijijini na vichoteo vilivyosalia vinaendelea kufanyiwa marekebisho vitakapokamilika mradi utahudumia watu zaidi ya wananchi 6000.

Aidha, Mbunge wa Chilonwa Mhe.Joel Mwaka amempongeza Naibu Waziri kwa kutembelea kijiji cha Itiso na kuangalia mradi wa maji uliokuwa ukisuasua tangu mwaka 2013 na kusababisha wananchi kutokupata maji katika kijiji cha Itizo kwa muda mrefu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...