Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia skimu kubwa ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni, kwa lengo la kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika kati ya Viongozi na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na wananchi wa vijiji vya Kata ya Mwamanyili Wilayani Busega kujadili juu ya mipango ya utekelezaji wa skimu hiyo.

Amesema katika Skimu hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Busega itaingia mkataba na kukopa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo tayari imekubali kutoa mkopo huo, ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye mashamba, kuwawezesha wananchi kununua mbegu bora, mbolea, na zana bora za kilimo.

Aidha, ameeleza kuwa wananchi katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha Ardhi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya  Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Ndg.Shadrack Yohana Mkazi wa Kijiji cha Nasa Ginnery Kata ya Mwamanyili,akichangia jambo katika kikao cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya ya Busega na wananchi kilichofanyika katika Kijiji cha Mwamanyili,  kwa lengo la kujadili juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...