Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Kampuni
ya Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya Bundesliga
mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia vipindi vya
startimes kwa wapenzi wa soka hapa nchini
Uzinduzi
huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa kuwafahamisha
wapenzi wa mpira kununua ving’amuzi na kujiunga na vifurushi ili
kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa
moja na startimes.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura
Hanif amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo
kufanya mashindano ya uandishi wa mechi hiyo na kwa mshindi wa
shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege kwenda moja kwa
moja Ujerumani.
Mkurugenzi
wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema
wana mahusiano mazuri na bundesliga kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano
na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.
Meneja
Uwendeshaji Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa huduma mpya ya
malipo kwa wale wenye hali ya chini wanaweza kulipia siku moja
king’amuzi cha Startimes kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo
kwa wiki utalipia elfu 4000.
Hata
hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema kuwa
ligi ya Bundesliga ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na ligi
zingine duniani kwa kuwa na wachezaji bora
Nae
Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa
kampuni ya startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara
mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe 18-27 Agosti mwaka huu
Makamu
wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa
ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto)
akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo
Mtangazaji
wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports
Bar', Shaffih Dauda akitoa uchambuzi pamoja na kubashiri ligi hiyo
itakavyokuwa kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.
Mhariri
mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu
ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka
2017/18 kwenye uzinduzi wa kuonesha ligi hiyo kwa mwaka wa tatu kupitia
kwenye king’amuzi cha Startames.
Mkurugenzi
wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza
kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu
kama Bundesliga
Picha ya Pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...