Nahodha wa timu ya Mchenga Mohamed Yusuph (jezi nyeupe) akiwa anajaribu kumtoka Nahodha TMT Isihaka Masoud katika mchezo wa pili wa fainali ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa TMT kuibuka na ushindi wa alama 87-78 dhidi ya Mchenga BBall Stars.


Fainali ya pili ya michuano ya mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings yameendelea tena kwa timu ya TMT kulipa kisasi kwa wapinzani wao kwa alama 87-78 dhidi ya Mchenga BBall Stars mchezo uliochezwa juzi katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay.


Katika mchezo wa fainali ya kwanza, Mchenga walifanikiwa kutoka na ushindi wa alama 101-70 vya TMT, lakini fainali ya pili TMT wamejibu mapigo na kuwaadhibu mahasimu wao na kuibua matumaini makubwa kwa kikosi na mashabiki wa timu hiyo.

Kwenye mchezo huo, TMT walionekana wako vizuri sana katiia idara zote ikiwemo ulinzi na ushambuliaji na kuwafanya Mchenga washindwe kufunga pale wanapofika langoni mwao na kuwafanya wacheze sana faulo

Mchenga timu inayosifika kuwa na wachezaji wazoefu na wakongwe walionekana kuchoka mapema sana na kutokuwa makini wakati wa kushambulia na kupoteza mipira mingi sana.

Nahodha wa Mchenga Mohamed Yusuph alioneka kusikitishwa na matokeo hayo na kuahidi kujipanga katika mchezo unaofuata na wataangalia ni wapi waliokosea ili wafanye marekebisho na kwenye michezo iliyobaki watahakikisha wanamaliza mapema.

Baada ya matokeo hayo, Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa mara nne ambapo fainali ya tatu itakuwa siku ya kesho Jumamosi na fainali ya nne inatarajiwa kuwa siku ya Jumatano na timu itakayotokea kushinda katika mechi hizo mbili mfululizo atatawazwa ubingwa wa Michuano ya Sprite BBall Kings 2017 na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 10 huku mshindi wa pili akipata Milioni 3 na mchezaji bora wa michuano hiyo (MVP) akizawadiwa milioni 2.

Michuano ya Sprite BBall Kings ilianza mapema Mwezi Mei na iliweza kusaili timu 54 na kuanza hatua za mtoano mwezi June katika Viwanja mbalimbali na imechukua takribani miezi mitatu kufikia Fainali, kwa mujibu wa waandaaji michuano hii itakuwa ni endelevu na wanatarajia mwakani kupata timu nyingi zaidi zitakazoshiriki.
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya TMT Lugano (Jezi Bluu) akijaribu kumtoka nahodha wa timu ya Mchenga Mohamed Yusuph  katika mchezo wa pili wa fainali ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa TMT kuibuka na ushindi wa alama 87-78 dhidi ya Mchenga BBall Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...