KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma mpya ya mawasiliano ya 4G LTE pamoja na kutambulisha huduma nyingine ya TTCL PESA.

Hata hivyo katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa mawasiliano bora yanahitajika ili kuendelea kuimarisha shughuli za kiuchumi mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko na bei nzuri kwa wazalishaji na Wakulima.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati akizindua huduma mpya ya kampuni ya Simu ya TTCL ya 4G LTE katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntika katika ofisi za Kampuni hiyo zilizopo jijini Mbeya.

Alisema mawasiliano bora yanamchango mkubwa katika ukuaji wa sekta za Elimu, Afya, Miundombinu, Biashara, utalii, huduma za jamii na sekta zingine mtambuka hivyo kitendo cha TTCL kuibuka upya kutasaidia kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa mbali na Mawasiliano kusaidia kukuza uchumi pia Wafanyakazi wa Sekta binafsi na sekta za umma wanahitaji mawasiliano bora ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo yao ya kazi.

Aidha alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa za kibiashara zinazotolewa na TTCL kama vile kuwa wakala wa kuuza vocha, Laini na kuwa Wakala wa huduma mpya ya kifedha ya TTCL Pesa kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ajira na vipato vyao.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kutoa kitambaa kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Afisa mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika baada ya kuzindua huduma ya 4G LTE mkoani MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kuonesha bango kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa 4G LTE mkoani Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...