Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemed(kulia)wakionyeshwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati) namba ya simu ya mshindi aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(kulia)akiongea kwa njia ya simu ya mkononi na mshindi aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa mkoa wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo,Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.Anaeshuhudia kushoto ni Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania, Mathew Kampambe.
Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo ambapo mkazi wa mkoa wa singida Munira Jumanne alijishindia Tsh. Laki 5/- Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.

Niwakati mwingine tena Vodacom Tanzania imewaletea wateja wake na watanzania wote kwa ujumla promosheni mpya kabambe kabisa inayojulikana kama Tusua Mapene. Promosheni hii itawawezesha wateja wetu na wananchi wote kwa wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki katika bahati nasibu na kujishindia vitita mbalimbali mpaka kiasi cha shilingi milioni 150 ndani ya siku 150.

Promosheni hii inampa mteja wa vodacom fursa ya kushiriki kupitia ujumbe mfupi wa maneno, huduma ya M-pesa au mitandao ya kijamii.

Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100M/-, washindi watano wa Sh. 20M/- na mshindi moja wa Sh. 15M/- KILA SIKU na mshindi wa mwisho wa promosheni(Grand draw) atajishindia kitita cha shilingi Million 150/-

Jinsi yakushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma neno “CHECK” au “VODA” kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu ikijumuisha kodi kwa kila ujumbe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mtu anatakiwa kufikisha kete ngapi ndo apate ata bonus ata ya Hiyo 20m au hata iyo 500000.

    ReplyDelete
  2. jamani tunaomba kujua tumecheza sana lakini hata senti tano hatujapata.huu mchezo ni wa kweli au tunazugwa.unatakiwa upate kete ngapi ndo upata hata kifyta jasho? hizo zawadi zinatolewa lini hata kwenye tv hatuonyeshwi? tafadhali tunaomba ufafanuzi

    ReplyDelete
  3. Ninaomba maelezo ili nishinde natakiwa nifikishe kete ngapi? Waliouliza kabla hawajajibiwa, naomba msipuuze. Nimecheza sana sioni chochote. Juzi ndio niliona washindi kwa Mara ya kwanza. Inakuwaje?

    Deo, Kahama

    ReplyDelete
  4. Maelezo ya namna ya kushinda hamjatoa. Au tunachangia mfuko kwanza?

    ReplyDelete
  5. Nimetumia pato langu lote la leo, hadi saa sita ucku nikiwa nimetumia kete za miezi Kitano bila kushinda! He, mshindi anapatikanaje?

    ReplyDelete
  6. Hii tahadhari mnayotoa, inaleta mashaka! Mbona hamtoi majibu ya maswali yaloulizwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...