Na Jacquiline Mrisho na Bushiri 
Matenda - MAELEZO.

Serikali imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea Serikali mapato. 

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.

Prof. Manyele amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kuagiza mzigo wa kemikali nchini.

“Natoa onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Prof. Manyele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...