Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAPEMA hii leo, upande wa Mashtaka katika kesi
inayomkabili raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), umeileza mahakama
kuwa, mshtakiwa huyo hana uhalali wa kuishi nchini ingawa imethibitika kuwa ni
kweli ana makazi eneo la mbezi jiji Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga amesema hayo mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ya mahakama iliyowaagiza kwenda kukagua makazi
ya mshtakiwa pamoja na hati ya mshtakiwa.
Amesema, kamishna wa Uhamiaji nchini amethibitisha
kuwa Tsampos, hana uhalali wa kuishi nchini ila Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Mbezi amethibitisha kuwa, mshtakiwa huyo ni kweli anayo makazi ya kuishi
eneo hilo.
Hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambole,
ameomba mahakama kumpatia dhamana mshtakiwa huyo kwani imedhihirisha kuwa ni
kweli mshtakiwa anaishi Mbezi na pia Kamishna wa Uhamiaji hajaeleza ni kwa nini
hana uhalali wa kuishi hapa nchini.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kwa ajili ya
kutolewa uamuzi kama apatiwe dhamana au la.
Raia huyo wa Afrika Kusini, anakabiliwa na mashtaka
ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na
kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.
Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61)akiwa amejificha sura yake katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...