Watu sita wakiwa ni wakazi wa sehemu mbalimbali wakiondoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, walipofika kwaajili ya kusomewa kesi inayowakabili ya kumiliki Meno ya Tembo kinyume ns sheria ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
 
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WATU sita wa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wamepandishwa kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya m.600 kinyume na Sheria.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Timon Vitalis amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Mohammed Laizer, mkazi Wa Mbagala Chamazi, Abubakari Zuberi, Wa Mbezi beach, Juma Salehe anaishi Manzese na Amor Shelukindo Wa Gairo Morogoro, 

Wengine ni Hamis Rashid, mkazi Wa Mbezi beach na Hamad Shaban ambo wote kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa mahakama hiyo.

Imedaiwa kuwa, Agosti 17 mwaka huu, katika eneo la Mbezi beach Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, watuhumiwa wote hao  walikutwa wakimiliki vipande 21 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 195000 abazo no sawa na milioni 437,190,000 mali ya serikali.
 
Pia mshtakiwa Laizer peke yake anadaiwa, siku hiyo hiyo katika eneo la Mbagala, alikutwa akimiliki vipande saba vya meno ya tembo vya pesa za kimarekani (USD )90,000 sawa sawa na shilingi milioni 201,780,000 mali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo wanadaiwa kukutwa na nyara hizo bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi Wa Wanyama pori.
Hata hivyo washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo.
 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kwahiyo umekamilika na kwa sasa wapo kwenye upelelezi wa mwisho ili shauli hili liende Mahakama Kuu kitengo cha uhujumu uchumi kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, 
Kesi hiyo itatajwa Septemba 7 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...