Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lulu Abbas maarufu kama "Luludiva" amekuwa akiendelea kujikusanyia lundo la mashabiki wa kazi zake kwa muda mfupi aliokaa kwenye game, ndani na nje ya nchi kutokana na jitihada zake katika muziki, huku nyimbo zake zikifanya vizuri katika media mbalimbali za hapa nchini, Afrika Mashariki, Nigeria, South Africa na Congo

Kwa Mara ya kwanza amefanikiwa kupata collabo ya kimataifa, akishirikishwa na msanii maarufu kutoka nchini Zimbambwe ambaye yupo chini ya label ya Military touch inayomilikiwa na msanii Jah Prayzah aliyefanya nyimbo na Diamond Platnum.

Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Lulu diva ameyazungumza haya, "Jah Prayzah najuana naye toka naenda South Africa kufanya video ya  nyimbo yangu ya pili ya Usimwache, aliniambia anakuja Tanzania akifika tuonane na alipofika alinitafuta na kuniomba nifanye collabo na msanii wake Exq ambaye yupo chini yake" alisema Lulu diva.

Aliendelea kusema kuwa "Alinisikilizisha nyimbo nikaiona ni nzuri na mimi naweza fanya kitu kizuri, kwa hiyo sikusita kutoa jibu nilikubali hapo hapo sababu niliona nitapata faida hasa kwa kuongeza kundi lingine la mashabiki kutoka Zimbabwe". 

Lulu diva alisema kuwa walifikia muafana na muandaaji huyo na kufanya nyimbo hiyo na muda wowote itaanza kusikika katika redio na televisheni mbalimbali hapa nchini.  hiyo anawaomba mashabiki wake wawe tayari kusikia na kuona.

Nyimbo hiyo imefanywa na Maproducer wakubwa watatu ambao ni
Producer wao: Tamuka huku kwa upande wa Tanzania ni: Abbydady, Tuddy Thomas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...