Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akizungumza na baadhi ya wakazi wa Bunju A mapema leo asubuhi,waliokuwa Wakimsubiri Kumueleza Changamoto zao Mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya soko la wa Wafanyabishara wa soko la Bunju A ambalo inaelezwa kuwa limechukuliwa na Muwekezaji.

DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Wananchi hao,ikiwemo changamoto ya eneo la Soko Bunju A,Mh Hapi amesema ametoa siku kumi 14  kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi, huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo  amepewa siku  tatu kuwasilisha nyaraka zake za umiliki.
 DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali,ambapo pia ametoa siku kumi 14  kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo  ametoa siku  tatu ampelekee nyaraka zake za umiliki
Baadhi ya Wakazi wa Bunju A wakimsikiliza DC Hapi alipokuwa akizungumza nao mapema leo na kusikiliza matatizo ya wananchi hao ikiwemo pia kuyapatia majibu.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wakazi hao wa Bunju A mapema leo asubuhi,yakiwa na jumbe za changamoto zao wakihitaji kutatuliwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...