Wabunifu 10 chipukizi kutoka sehemu mbalimbali nchini wamaechaguliwa kuingia katika shindano la kumi la kumtafuta mbunifu chipukizi bora lililopewa jina la “SFW Washington Benbella Emerging Designer Competition.”washiriki hao wametoka katika jumla ya washiriki 30 walituma maombi yao, na watapatiwa nafasi ya kuonesha nguo zao katika maonesho ya SWAHILI FASHION WEEK & AWARDS yatakayofanyika tarehe 1, 2, 3 mwezi December jijini Dar es Salam nchini Tanzania.

“Awamu ya kumi ya mashindao ya kumtafuta mbunifu chipukizi wa mwaka yamekuwa ya aina yake, si tu kiushindani bali ni ya kushangaza. Washiriki hawa kumi wamebeba sifa ya kuenzi dhamira ya maonesho ya mwaka huu. Macho na masikio yote ya washabiki wa mitindo yapo wazi kutazama mavazi ya kipekee katika kusherekea maadhimisho ya miaka kumi ya Swahili fashion week. Tunaomba kila mtu aweze kufika kushuhudia dunia mpya ya mitindo kutoka kwa watu wabunifu wapya katika setka ya mitindo.” Alisema Glory Urassa Afisa Mradi wa Swahili Fashion Week.

Kamati ya uchaguzi wa mwaka huu, iliundwa na mbunifu Jamilla Vera Swai, mbunifu Samuel Zebadayo, pamoja na mwanamitindo Rio Paul, walivutiwa na michoro ya kipekee na vitambaa vyenye ubora kutoka kwa vijana wenye hasira ya kutawala sekta ya mitindo.

Kwa miaka kumi iliyopita ,toka kuanzishwa kwa mashindano haya mwaka 2008, yamewza kukusanya Zaidi ya vipaji vichanga elfu moja kutoka sehemu mbalimbali afrika ambao wanaendelea kufanya kazi ya mitindo, kufungua nembo zao na kuonyesha mitindo yao katika majukwaa mbalibali duniani. Wafuatao ni washindi waliopita Shaabaz Sayeed (2016), Kulwa Mkwandule (2015), Medrad Mlowe (2014), Bhoke Chacha (2013), Philista Onyang’o (2012), Subira Wahure (2010), 2jenge Africa Mataley (2009) and Edwin Musiba (2008).

Kamati ya majaji ilikaa na kuchagua awamu ya kwanza ya watu kumi amabo ni Liberatha Alibalio, Charity Nyaimaga, Maryimmaculate Gervace, Emmanuel Kisusi, Agness Sixbeabeatus, Mohammed Juma, Anjali Borkhataria, Edina Ibrahim, Gisela Kaguo, na Jackline Ottaru. Mchakato wa kutaendelea hadi pale atakapopatikama mshindi mmoja tu wa mashindano haya, ambaye atapewa tuzo katika siku tatu na ya mwisho ya maonesho ya Swahili Fashion Week 2017, yatakayofanyika  Makumbusho ya Taifa kuanzia tarehe 1 hadi 3 mwezi disemba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...