Na Karama Kenyunko
WAKILI wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Msuya, Miriam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40), ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuita Afisa wa upelelezi makosa ya jinai wa Temeke,(RCO) aje aeleze upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi.

Wakili Peter Kibatala amedai hayo leo mbele ya Hakimu  Mkazi Thomas Simba baada ya wakili wa Serikali Estazia Wilson kudai kesi hiyo leo ilikuja kwaajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Simba amekubaliana na ombi hilo la upande  wa  utetezi na kusisistiza kuwa RCO aitwe mahakamani hapo Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 16,2017 kwa ajili ya kutajwa.

Februari 23, mwaka huu, washtakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey  Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.

Katika kesi hiyo namba 5/2017 inadaiwa Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa walimuua dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...