Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto),
akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa
Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es
Salaam jana. Mkurugenzi huyo alisema katika maadhimisho hayo NBC imezidi
kuboresha ubora wa huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja
wao wa kada zote. Kulia ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi wakikata utepe ili kurusha ‘puto’
kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika
Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC
jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia),
akizungumza waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wafanyakazi wa
benki hiyo katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate
jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...