JUMUIYA ya raia wa Comoro waishio Tanzania wameiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini kusaidia kupatikana kwa ndugu yao Ammar Abdousoi Madou (26) aliyepotea na kutoweka kusikojulikana tangu tarehe 29 Juni mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo (jana) Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Jumuiya hiyo, Larifou Said alisema taarifa za kupotea kwa Madou ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda ziliifikia familia yake tarehe 29 Juni, mwaka huu.

Said anasema familia ya Madou ilipokea taarifa za kushikiliwa kwa Madou na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha tarehe 27 Juni, mwaka huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa Madou anaeishi Mkoani Arusha na baadae kuelezwa kuwa aliachiwa huru tarehe 29 Juni mwaka huu, ingawa tangu kipindi hawajaweza kuonana nae hadi sasa.

Anasema pamoja na familia hiyo kufanya jitihada mbalimbali za kufanikisha upatikanaji wa ndugu yao ikiwemo kufanya Mawasiliano ya mara kwa mara na vyombo vya usalama ikiwemo kuwasiliana na Idara ya upelelezi ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufahamu undani na sababu ya kukamatwa kwa Madou.

Mwanasheria wa Jumuiya ya Raia wa Comoro waishio Tanzania, Larifou Said akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu tukio la kupotea kwa Mwanafunzi Raia wa nchi hiyo Ammar Abdousoi Madou (pichani) ambapo waliliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu yao huyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...