Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Wamesema wana ushirika walijitahidi kutuma mwenyekiti wa Kijiji hicho kufuatilia upotevu huo bila mafanikio jambo lililowakatisha tamaa ya kuendelea na ushirika.

Dkt Nchimbi amesema “moja ya Muhimili wa mafanikio ya kilimo cha pamba ni ushirika ulio imara, tunakoelekea kwenye kilimo cha pamba chenye tija hawa wasiowaaminifu kwenye bodi watatukwaza na kutukwamishwa, kama bodi haifanyi kazi vizuri kwanini iendelee?, Mkuu wa Wilaya naimani kwa utendaji wako mzuri hili halitachukua zaidi ya wiki mbili”.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Katibu Tawala Wilaya ya Iramba Pius Songoma akishiriki kuwaelekea wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa zawadi ya kilo tano za mbegu ya pamba aliyopewa.
Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain itakayosambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida akizungumza na wakulima wa zao hilo Katika kijiji cha Msai Wilayani Iramba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...